Posti Ya Haji Manara Mara Baada Ya Ngoma Kusaini Mkataba Azam Fc.


Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa Ngoma hakuwa mgonjwa bali ilikuwa ni kukosa mishahara ndiyo sababu iliyokuwa ikimfanya asicheze.

Kauli hiyo ya Manara imejili mara baada ya taarifa kuenea kuwa tayari straika huyo amesaini mktaba wa awali na klabu ya Azam fc.

Manara kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe unaosomeka.

Donald Ngoma na @azamfcofficial wamemalizana rasmi...inavyoonekana Ngoma hakuwa mgonjwa wa afya bila shaka alikuwa mgonjwa wa kukosa mishahara.....sijui hajalipwa miezi mingapi maskini ya God...kila la kheri kwako Striker @donaldngoma11

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.