Haji Manara Hajawaacha Salama 'YANGA' Kwa Swala La Mchezaji Huyu
Msemaji wa klabu ya Simba, "Haji Manara" amefunguka na kuwajia juu baadhi wa watu ambao wamekuwa wakotoa taarifa zinazoaminika kuwa na za Upotoshaji Kuhusiana na Uraia wa Beki wa klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi, Paul Bukaba.
Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa Bukaba ni mtanzania halali mwenye uraia na alikwenda nchini Burundi kucheza Soka tu.
Na kama ilivyo ada kwa Manara hakuacha kuwashutumu watu ambapo katika taarifa hiyo amewabebesha mzigo huo watani wa jadi wa Simba huku akiwaita jina ambalo kwa haraka kulitambua ni Vigumu "NDEGELEC"
"Tunazo taarifa za hovyo zinazosambazwa eti mchezaji wetu huyo ni Mrundi na hvyo tutakatiwa rufaa dhidi ya Wadjibout.. Poul Bukaba ni mtanzania na Urundi alienda kucheza Soka tu na anamiliki uraia wa kuzaliwa wa Tanzania...tafuteni lingine hili mmenoa na pia hangaikeni na yenu ikiwemo kulipa mishahara ya wachezaji wenu....Ndegelec"
Jambo la kufahamu mpendwa msomaji wa "Sokakiganjani blog" ni kwamba Bukaba alijiunga na Imba Msimu uliopita Akitokea Klabu ya Athletico Olympic inayoshiriki ligi kuu nchini Burundi.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.