RAGE ATAJA SIRI YA UBINGWA SIMBA
Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ametaja mshikamano baina ya viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki ndio ngao iliyowafanya kutwaa ubingwa.
Simba ilitawazwa mabingwa wapya wa ligi kuu msimu wa 2017/18 jana baada ya watani wao wa jadi Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons hivyo kushindwa kufikia alama 65 walizo nazo.
Rage amesema ukiacha ubora wa kikosi walichonacho msimu huu pia mshikamano ulichangia kufikia hatua hiyo kwakua kila mtu alitimiza majukumu yake.
"Wachezaji walijituma uwanjani, viongozi waliwapa mazingira mazuri, benchi la ufundi lilifanya kazi vizuri pamoja na mashabiki ambao walikuwa wakijitokeza kwa wingi viwanjani," alisema Rage.
Simba imetwaa ubingwa ikiwa imesalia na mechi tatu ambapo kesho itashuka katika uwanja wa Namfua mkoani Singida kucheza na Singida United.
Wekundu hao ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wa ligi mpaka sasa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.