Yanga Haijakata Tamaa Kumnasa Straika Mtogo.
Yanga imekuwa kwenye mazungumzo na Straika wa Wolaita Dicha Djako Arafat raia wa Togo ambaye ni mchezaji pekee wa Kimataifa katika klabu hiyo.
Yanga ilianza mazungumzo na mchezaji huyo baada ya kukamilika kwa mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho hatua ya mtoano, mchezo ulioipa Yanga tiketi ya kutinga hatua ya makundi.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Husseni Nyika amethibitisha juu ya azma ya Yanga kutaka kumsajili straika huyo.
Djako ndiye kinara wa upachikaji mabao katika klabu ya Wolaitta Dicha akiwa ameifungia timu hiyo mabao saba mpaka sasa.
Ndiye aliyefunga bao pekee la Dicha kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga
Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 huenda akasajiliwa kwa ajili ya msimu ujao kwani hana sifa za kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi kwa kuwa tayari ameitumikia Dicha katika michuano hiyo msimu huu.
Yanga imedhamiria kusuka upya kikosi chake baada ya kushindwa kutetea ubingwa uliochukuliwa na Simba msimu huu.
Mbali ya Djako, mshambuliaji raia wa Nigeria Quadri Kola Aladeokun kutoka Mbabane Highlanders naye anasaka nafasi ya kusajiliwa na Yanga
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.