Kabwili Out Under 20
Kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' Ammy Ninje amesema ameagiza mlinda lango kutoka visiwani Zanzibar kuchukua nafasi ya Ramadhani Kabwili.
Kabwili yuko kwenye kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kusafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo dhidi ya USM Alger.
Akihojiwa na Azam TV jana, Ninje amesema baada ya mchezo wa marudiano dhidi ya DRC, aliwapa wachezaji mapumziko ya siku nne.
Amedai Yanga haikufuata taratibu kumjumuisha Kabwili kwenye kikosi chake kilichocheza na Simba mwishoni mwa wiki, Kabwili akiwa miongoni mwa wachezaji wa akiba.
Hata hivyo Kabwili amelazimika kujumuishwa katika kikosi cha Yanga baada ya kuumia Benno Kakolanya.
Ngorongoro Heroes inajiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON U20 2019 dhidi ya Mali May 13 .
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.