lechantre afichua mbinu za ubingwa Simba sc


Na Joseph michael

-Simba inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 62 katika mechi 26 ilizocheza msimu huu ikifuatiwa na Azam (49) na Yanga (48).

 -Licha ya kubakiza pointi tano tu ili kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa Simba Pierre Lechantre amesema kazi inayomkabili ni kubwa kutimiza ndoto hiyo.

-Simba inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 62 katika mechi 26 ilizocheza msimu huu ikifuatiwa na Azam (49) na Yanga (48).

-Timu hiyo ina mechi nne mkononi dhidi ya Ndanda, Kagera Sugar itakayocheza nyumbani kabla ya kuzifuata ugenini Singida United na Majimaji ya Songea.

-Lechantre alisema pointi hizo ni chache, lakini Simba inatakiwa kufanya kazi ya ziada kupata ushindi kwa kuwa wapinzani wao siyo timu za kubeza.

-Mfaransa huyo alisema wanatakiwa kuendeleza kasi waliyoanza nayo mwanzo kupata matokeo mazuri, vinginevyo wapinzani wao wanaweza kuwakwamisha.

-“Mechi zilizobaki ni ngumu siyo rahisi ni sawa na mtu anapoanza kupanda mlima, anaanza kwa kasi, lakini anapokaribia kumaliza anakuwa amechoka sana.

-“Sisi hatutakiwi kuchoka kasi tuliyoanza nayo inapaswa kuendelezwa. Mechi zote kwetu ni ngumu na muhimu,” alisema Lechantre.

-Lechantre alisema mtihani wa kwanza ni kushinda mechi mbili za mwanzo ambazo anaziandalia mbinu za kuhakikisha anapata pointi sita. Simba inatakiwa kufanya maandalizi ya kutosha katika mechi nne zilizobaki ambazo zinaweza kuigharimu endapo haitafanya maandalizi mazuri.

-Endapo Simba itapoteza pointi au kutoka sare katika mchezo wa kwanza kati ya mechi zilizobaki inaweza kuanza kucheza kwa presha kubwa mechi zinazofuata.

-Timu hiyo inaweza kupata mtihani katika mechi mbili dhidi ya Singida United na Majimaji ambazo itakuwa ugenini kwenye viwanja tofauti vya Namfua na Majimaji Songea.

-Pia ina mechi mbili ngumu nyumbani dhidi ya Kagera Sugar na Ndanda ambazo katika siku za hivi karibuni zimeonyesha kuimarika kulinganisha na mzunguko wa kwanza.

Rekodi

-Simba katika mechi ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Ndanda ilishinda mabao 2-0, kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Timu hiyo ikiwa ugenini iliinyuka Kagera Sugar mabao 2-0, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

-Simba iliifunga Singida United mabao 4-0 kabla ya kuigagadua Majimaji 4-0 na mechi zote zilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.