Straika mpya simba Okwi anakaa


By Saddam Sadick

-Boniventure ndiye straika pekee wa timu za nje ya 10 bora, ambaye amefunga mabao zaidi ya 10, rekodi ambayo inamfanya kuwa mchezaji wa kuogopwa zaidi Ligi Kuu Bara.

-REKODI za straika, Marcel Boniventure anayekaribia kutua Simba zimeanza kuwatisha mastaa wa timu hiyo, Emmanuel Okwi na John Bocco kwenye safu ya ushambuliaji.

-Boniventure ndiye straika pekee wa timu za nje ya 10 bora, ambaye amefunga mabao zaidi ya 10, rekodi ambayo inamfanya kuwa mchezaji wa kuogopwa zaidi Ligi Kuu Bara.

-Straika huyo wa Majimaji ya Songea ana mabao 13 Ligi Kuu, akishika nafasi ya tatu kwa ufungaji nyuma ya Okwi mwenye 19 na nahodha wa Simba, John Bocco mwenye 14.

-Boniventure, ambaye alilelewa na timu ya vijana ya Simba kabla ya kutua Majimaji, ameweka rekodi ya aina yake baada ya kufunga mabao saba katika mechi nne alizocheza mwezi Aprili, hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi huo.

-Rekodi hiyo imewagusa mabosi wa Simba ambao, tayari wameanza kuzungumza naye japokuwa mwenyewe anasema kuwa, ana ofa nyingi mezani na huenda akatimkia nje ya nchi ambako kocha wake wa zamani, Kally Ongala anamuunganishia.

-Mabao 13 ya Boniventure ni sawa na yaliyofungwa na nyota watatu wa Yanga, Ibrahim Ajibu mwenye saba, Pius Buswita mwenye manne na Donald Ngoma mwenye mabao mawili.

-Straika pekee wa Yanga anayemkaribia kwa mabao ni Obrey Chirwa aliyefunga 12, lakini kwa timu kama Azam FC hakuna hata staa yeyote anayemkaribia.

-Staa huyo pia amekuwa straika watatu kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja ‘Hat Trick’ akifanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting wikiendi iliyopita. Wengine walioweza ni Okwi aliyefunga dhidi ya Ruvu Agosti mwaka jana na staa wa Yanga, Obrey Chirwa aliyefunga dhidi ya Mbeya City.

MSIKIE MWENYEWE
-Akizungumza na Mwanaspoti, Boniventure alisema kazi yake ni kucheza mpira, hivyo iwapo Simba watampa ofa ya maana, basi yupo tayari kujiunga nao.

-Alisema hadi sasa amepata ofa ya kwenda nchini Sweden kwa ajili ya majaribio baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu na kwamba, anaamini atafuzu.

-“Simba tayari wameonyesha nia ya kunihitaji kwa sababu tumeshazungumza, kwa hiyo kama maslahi yao yanashawishi nitakwenda huko, lakini kikubwa nataka kuendeleza kipaji changu kwa kucheza na timu ambayo nitapata namba ya mara kwa mara,” alisema Boniventure.

-Aliongeza kuwa zaidi anatamani kucheza soka nje ya Afrika, hivyo akifuzu majaribio nchini Sweden atatimkia huko kwani, ameshaweka mkakati wa kutoichezea tena Majimaji.

-“Mipango yangu ni kucheza soka la kulipwa nje ya Afrika, nataka nicheze Ulaya ili kujitangaza zaidi, hata Simba nitajiunga nao kutokana na dalili zao za kutwaa Ubingwa kwani, mwakani lazima wacheze anga za kimataifa,” alisema kinda huyo.

-Simba imeanza usajili wake kwa ajili ya kujiimariasha na mechi za Ligi Kuu msimu ujao pamoja na michuano ya kimataifa, endapo watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. Simba na Majimaji zitamaliza ligi msimu huu.

Joseph michael @

Kutoka mwanaspoti

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.