MASOUD DJUMA AKABIDHIWA TIMU

Masoud Djuma lined up to replace Hans van Pluijm at Singida United
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye michuano ya SportPesa, inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Kenya.

Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa, wataachana na Kocha wao Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre, baada ya Ligi ya msimu huu kumalizika Jumatatu ya wiki inayokuja.


Taarifa hizo zinadai kuwa, uongozi umeona mshahara wa Mfaransa huyo ni mkubwa sana ikilinganishwa na uwezo wake, hivyo wanafikiria kuachana naye.

Mfaransa huyo, ambaye alisaini mkataba wa miezi sita inayomalizika mwezi ujao, huenda akatimkia Cameroon, ambako ameomba kibarua cha kuinoa timu ya Taifa ya nchini humo, kama Simba wataamua kuachana naye.

Kigogo mmoja ndani ya timu hiyo ameliambia DIMBA Jumatano kuwa, kwa sasa akili zao ni kutafuta mbadala wa Mfaransa huyo, ili asaidiane na Djuma.

“Ni kweli kuna uwezekano mkubwa tukashindwa kuendelea na Pierre (Lechantre), kwani mshahara wake ni mkubwa sana, tunachofikiria ni kutafuta kocha mwingine mkuu, lakini mwenye uwezo mkubwa.

“Baada ya kumalizika kwa Ligi, timu itakuwa na maandalizi ya kwenda Kenya kushiriki michuano ya SportPesa na kocha wetu msaidizi Masoud Djuma ndiye atakayebeba jukumu hilo"
alisema.

-DIMBA Jumatano lilimtafuta Mfaransa huyo ili kuzungumzia hatima yake, hakuwa na mengi zaidi ya kusema yeye kwa sasa hawezi kusema lolote, kwani mambo yake yanasimamiwa na mawakala wake.

“Kwa sasa siwezi kusema mengi, kwani ninao mawakala wangu wanaoshughulikia mambo yangu, nadhani kila kitu kitakuwa wazi,” alisema.

Source: Dimba

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.