Tetesi Za Usajili Ligi Kuu Ya Tanzania Bara Vodacom Premier league 23/05 /2018
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Donald Ngoma amesema wazi kuwa yupo tayari kuondoka katika klabu yake ya Yanga endapo watafikia makubaliano maalumu pia kuna taarifa za chini chini kuwa kuna klabu inamtia kiburi mchezaji huyo ili wavunje mkataba wake
Imeripotiwa kuwa klabu ya Azam fc imeanza harakati za usajili mapema kwa kuwatolea macho Adam salamba, Mohamed Ibrahim Mo na Ramadhani chizya Kichuya ni miongoni mwa wanaowataka kuwasajili ili kuimarisha kikosi chao
Lakini klabu ya yanga ipo tayari kujiondoa kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Lipuli fc Adam salamba baada ya vilabu vya Simba na Azam fc kumtolea macho
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga sc Obrey Chirwa imeripotiwa ananyemelewa na mahasimu wao wa jadi Simba
Imeripotiwa kuwa mchezaji wa Yanga sc Haji Mwinyi ngwali huenda akawakacha mabosi wake na kutimukia katika klabu ya fc leopard ya nchini Nairobi Kenya
Simba sc wanataka kumsajili mshambuliaji wa maji maji Marcel bonaventure taarifa za awali zinasema tiyari wapo kwenye mazungumzo
Hata hivyo klabu ya Singida United upo katika hatua za mwisho mwisho wa mazungumzo na Etiene ndayijage ili kukinoa kikosi cha Singida United mda wowote kuanzia sasa anaweza kutangazwa kocha mkuu wa Singida United
Pia klabu ya Mbao Fc imevunja ukimya hii ni baada ya vilabu vikubwa vitatu vya Ligi kuu ya Tanzania bara Vodacom kuhitaji huduma ya mshambuliaji wao habib kiyombo na kusema kuwa hawapo tiyari kumuuza nyota huyo kwa dau lolote lile
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.