CAF YAWABADILISHIA RATIBA SIMBA SC.

Tokeo la picha la masoud djuma
-Shirikisho la soka la Africa (CAF) limefanya mabadiliko ya kalenda ya michuano inayoandaliwa na CAF ile ya Caf Champions League na Caf Confederation CUP michuano hiyo ilikuwa inafanyika mwezi wa Pili (february) hadi Mwezi wa kumi na moja (November)

-Sasa badala ya February hadi November michuano hiyo itakuwa inachezwa kuanzia mwezi wa August hadi May kama michuano ya ulaya inavyoachezwa sababu kubwa waliyosema CAF michuano hiyo ichezwe wakati ligi za nchi husika zikiwa zinachezwa.


-Ila msimu ujao Michuano hiyo itachezwa kuanzia mwezi December mara baada ya kumalizika mashindano ya mwaka huu yanayoisha mwishoni mwa mwezi November. Baada ya kuisha mashindano ya msimu huu yataanza December 2018 na yataisha May 2019 pia mechi zake zitakuwa zinachezwa katikati ya wiki badala ya wikendi.

-Babadiliko hayo ya kalenda ya CAF pia yamebadilisha michuano ya Afcon (Africa Cup of Nation) kuanzia msimu ujao michuano hiyo ilikuwa inachezwa mwezi January na sasa michuano hiyo itakuwa inafanyika Mwezi July na mashindano ya msimu ujayo yatafanyika July 2019.

-Klabu ya Simba mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara watashiriki klabu bingwa Afrika (Caf Champions League) msimu ujao na wataanza December hadi May ni muda kwa klabu hiyo kufanya usajili mzuri na maandalizi mazuri ya mashindano hayo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.