ILE ISHU YA NYOTA WA YANGA KUTIMUKIA KENYA IKO HIVI
Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga Sc, Haji Mwinyi yuko mbioni kujiunga na klabu ya AFC Leopard ya Kenya. Haji Mwinyi anasubili mechi za ligi kuu ziishe ili aweze kusepa zake Kenya.
-Hii si mara ya kwanza kwa beki huyo wa kushoto kutaka kujiunga na klabu ya AFC Leopard kwani baada ya kumalizika kwa mashindano ya kombe la Cecafa aliandika barua ya kuomba klabu ya Yanga imuache awe huru ili ajiunge na klabu hiyo.
-Wakala wa mchezaji huyo Mwinyi Mgwali ambaye ni baba yake amedai walishafanya mazungumzo na AFC Leopard na mambo yameenda poa kwa sasa wanasubili kumalizika kwa mechi za ligi kuu ili awasiliane na klabu ya Yanga kuhusu kumuachia beki huyo.
-Haijajulikana Haji Mwinyi ataondoka vipi Yanga kwani bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Yanga. Mwinyi ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2015/16 amecheza Yanga kwa misimu mitatu amedai anataka kwenda nje ya nchi kucheza soka.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.