Kocha Taifa Stars Kubeba Mikoba Ya Pluijm Singida United.

Kocha mpya wa timu ya Singida United, Hemed Morroco amesema mtangulizi wake Hans van Pluijm alifanya kazi kubwa kuiweka kwenye ramani ya soka nchini licha ya kuwa wageni kwenye ligi.

Morroco ametambulishwa jioni ya leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali wa kombe la FA waliolala kwa mabao 3-2 kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema anajua anakwenda kuvaa viatu vya kocha bora lakini amehitaji ushirikiano kutoka kwa Uongozi, wachezaji, wapenzi na mashabiki ili kuisogeza mbele timu hiyo.

"Pluijm ni kocha mzuri namheshimu sana kwa kazi kubwa aliyofanya lakini naamini nitafanya vizuri ninachohitaji ni ushirikiano," alisema Morroco.

Pluijm amejiunga na timu ya Azam FC na tayari ataondoka na matajiri hao kurejea Dar es Salaam kuja kumalizana.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.