Rais Mtarajiwa Yanga Ampa Tuzo Emmanuel Okwi.
KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ‘Mzee Akilimali’ amesema kwake anaona mchezaji bora wa kigeni msimu huu ni Emmanuel Okwi.
Okwi ameipa Simba ubingwa msimu uliopita baada ya kupita miaka mitano bila kufanya hivyo huku akiibuka mfungaji bora wa ligi kuu akiwa katupia kambani mabao 20.
Mzee Akilimali ambaye amepanga kuwania Urais wa Yanga, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Okwi alikuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho na kusaidia kutwaa ubingwa huku yeye akifunga mabao mengi huku akimtaka asibadilike na kurejea tabia ya zamani ya kuomba ruhusa mara kwa mara.
“Kwa wachezaji wa kigeni msimu huu Okwi ndiye mchezaji bora, alifanya vizuri baada ya kuisaidia timu itwae ubingwa na alikuwa tishio kila alipokuwa akiingia uwanjani kuwakabili wapinzani na hata mashabiki pinzani waliogopa kutokana na uwezo wake.
“Lakini ushauri wangu ni kwamba asije akayarudia yale ambayo yaliwahi kutokea huko nyuma siyo anapewa ruhusa siku tano yeye anakaa 20 haifai ajue yuko kazini na klabu yake inamthamini ndiyo maana akawa pale. Kwa Yanga sijaona mchezaji wa kimataifa aliyefanya vyema kwa kuwa wengi walikuwa majeruhi,” alisema Akilimali.
Okwi alipotua Simba msimu uliopita alipewa Sh136 huku Championi Jumamosi likidokezwa kwamba nyumba yake anayoishi Dar es Salaam analipiwa zaidi ya Shilingi milioni 2 kwa mwezi
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.