Tshishimbi Aitilia Mashaka Yanga, Asema Hana Uhakika Kama Ataongeza Mkataba.


Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi amesema hana uhakika kama ataongeza mkataba wa kuitumika klabu hiyo endapo utamalizika.

Tshishimbi ambaye alijiunga na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Mbabane Swallows amesema kuwa hana uhakika ya kuwa ataongeza mkataba wa kuendelea kuitumika klabu hiyo licha ya kuwa anatamani kutwaa ubingwa akiwa na klabu hiyo.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa anatamani kutwaa ubingwa akiwa na Yanga na kuongeza kuwa angependa timu hiyo ifike angalau nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).



“Nahitaji kuendelea kukaa hapa kwa sababu sijafikia malengo yangu, nahitaji kutwaa ubingwa nikiwa na Yanga nabpia nahitaji angalau kutinga hatua ya Nusu fainali ya CAF Confederation Cup,” Tshishimbi.
Mkataba wa Tshishimbi unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.