Nilishafanya Mengi Kwenye Muziki, Acha Sasa Iwe Zamu ya Mpira:-Alikiba .


Nilishafanya Mengi Kwenye Muziki, Acha Sasa Iwe Zamu ya Mpira:-Alikiba
Mwanamuziki Alikiba mbae kwa sasa amegeuka na kuingia katika mpira anasema kuwa amekuwa akifanya muziki kwa muda mrefu huku kipaji chake cha kucheza mpira akiwa hakifanyii kazi yoyote na hivyo anaona kuwa sasa ni wakati wa mpira.

Akiongea na waandishi wa habari, Alikiba anasema kuwa kwa muda sasa amefanya mengi katika muziki na amepokea tuzo na vitu vingi katika muziki hivyo, ndoto kubwa aliyonayo sasa hivi ni kujituma katika mpira ili apate tuzo ya kujiamisha kuwa ana kipaji cha mpira pia

lengo ni kufanikisha na kupata medali ya tuzo katika mpira,ili nihisi kama nimepata kitu ili niamini kuwa nina kipaji  cha mpira na cha kuimba kwa sababu kwenye muziki tayari nilisha fanya mambo mengi na kupokea vitu vingi kwaio sasa hivi ni zamu ya football.
Hata hivyo alikiba nasema kuwa katika mpira bado naendelea kuangalia nani ni role model wake pamoja na kwamba anawaona wapo wengi wanafanya vizuri lakini anasisitiza zaidi katika mazoezi na kujituma

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.