Mzambia wa Simba aanza cheche baada ya ITC yake kutua nchini asema haya.
Claytous Chama |
MARA baada ya kibali chake kupatikana, kiungo mchezeshaji wa Simba ambaye ni raia wa Zambia, Claytous Chama amesisitiza kwamba anakuja na moto wa hatari.
Chama alishindwa kuichezea Simba kwenye michezo yake miwili ya mwanzo wa ligi kutokana na klabu yake ya Power Dynamos aliyokuwa anaichezea kabla ya kutua Simba kushindwa kutuma ITC yake kwa wakati. Alikosa michezo ya Simba dhidi ya Prisons na Mbeya City.
Akizungumza na Spoti Xtra, kiungo huyo ambaye kwa sasa ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ amesema ; “Kila kitu kimeenda sawa na nitaanza kucheza hivi karibuni. Kwangu ni jambo zuri kwani nitaanza majukumu katika klabu yangu mpya, niseme tu wazi nitapambana kuona klabu yangu inafanya vizuri kwenye mechi zake, wengi wasubiri kuona ni nini ambacho nitafanya kwa ajili ya timu
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.