Deal Done: Zahera kitanzi miaka miwili Yanga


Mashabiki na mabosi wa Yanga sasa watapata usingizi na akili zao kutulia baada ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kusaini rasmi mkataba wa kukinoa kikosi hicho.


Tangu ametua nchini, Zahera amekuwa akifanya kazi bila kuwa na mkataba, lakini leo Ijumaa jioni Mkongo huyo ametia wino mkataba wa miezi sita kuwanoa mabingwa hao wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.


Lakini, Mwanaspoti ambalo limeshuhudia Mkongo huyo akimwaga wino, linafahamu kuwa kuchelewa kusaini mkataba huo ni sehemu ya makubaliano yake na mabosi wa Yanga.


Pia, Mwanaspoti linafahamu kuwa mara baada ya kusaini mkataba huo, Zahera alikwea pipa kwenda kwao DR Congo na atarejea ndani ya siku chache zijazo kuendelea na majukumu yake.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.