Kumbe Issue Ya Salamba Yanga Walifanyiwa Figisu..


Uongozi wa klabu ya Yanga umelalamikia kuingiliwa katika usajili wa mshambuliaji wa Lipuli FC, Adam Salamba na kukwamisha dili hilo.

Mapema wiki hii Uongozi wa Azam FC ulithibitisha kutaka kumsajili mshambuliaji huku wakituma barua kwa Lipuli kutaka saini ya nyota huyo.

Jana Uongozi wa Lipuli ulitoa barua kuwa haitaweza kumruhusu Salamba kwenda Yanga kwakua ni kinyume cha kanuni ya FIFA, CAF na TFF kuwa mchezaji huyo atakuwa amechezea timu tatu ndani ya msimu mmoja.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,  Boniface Mkwasa amesema imekuwa kawaida sasa kwa kila mchezaji wanaomtaka kunatokea timu nyingine kwa ajili ya kuwaharibia.

Mkwasa amesema lengo lao ni kumsaidia mchezaji kwa kumtangaza kwenye michuano ya Shirikisho Afrika lakini timu nyingine zinapenda kuiharibia Yanga.

"Utaona Yanga tukihitaji mchezaji timu nyingine zikiingilia kati kutaka kutuharibia lakini bado tutaendelea kuongea na wenzetu wa Lipuli kuangalia uwezekano wa kumpata Salamba," alisema Mkwasa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.