WAMBURA AIBURUZA TFF MAHAKAMA KUU

Wambura
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura ameiomba Mahakama kuu kukubali marejeo ya hukumu yake dhidi ya kamati za TFF ya kufungiwa maisha kutojihusisha na soka.

Wambura alifungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka baada ya kukutwa na makosa matatu hali iliyopelekea kupoteza nafasi yake ndani ya TFF.

Hukumu kwenye shauri namba 20/2018 imetolewa leo tarehe 18/5/ 2018 na jaji Wilfred  Ndyasobera baada ya kuridhia hoja za mawakili wa Wambura, Masumbuko Lamwai na Emmanuel Muga.

Maamuzi hayo yanatokana na maombi yaliyowasilishwa Mahakama kuu wiki mbili zilizopita yakiomba Mahakama imruhusu Wambura kufungua kesi ya msingi kuomba kutengua maamuzi ya kamati za TFF.

Maombi ya mapitio yaani Judicial Review ni haki ya msingi inayotafutwa pale chombo kilichotoa maamuzi kilivunja sheria au kukiuka misingi ya haki kama haki ya kutosikilizwa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.