VIDEO: Haji Manara Awapa Pole Yanga, Awambia Haya

Uongozi wa klabu Simba umesema kukosa taji la VPL msimu huu itakuwa ni muujiza, huku Msemaji wake Haji Manara akitoa pole kwa Yanga kwa kuupoteza ubingwa huo na kufungwa 4-0 na USM Algers. Manara alikuwa akizungumza na Mshikemshike Viwanjani kuelekea mechi ya Mei 12 mwaka huu dhidi ya Singida United Uwanja wa Namfua. Katika hatua nyingine, Haji Manara amewapiga vijembe watani wao wa jadi Yanga ambao kwa asilimia kubwa wanaelekea kuwavua ubingwa wa VPL waliotwaa mara tatu mfululizo. Yanga wamechapwa mabao manne kwa sifuri na USM Alger ya Algeria kwenye mechi ya kwanza ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.