Simba Kushuka Dimbani Leo Kusaka Pointi Tatu Dhidi Ya Timu Ngumu.


Baada ya kuibuka na ushindi katika michezo mitatu mfululizo dhidi ya Njombe Mji, Mtibwa na Mbeya City, klabu ya Simba inatarajiwa kushuka dimbani kusaka ushindi mwingine dhidi ya Prisons ili kuuukaribia zaidi ubingwa.

Simba ambayo kwa sasa ipo kileleni mwa ligi kuu ikiwa mbele kwa pointi 8 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Yanga ambao wapo katika nafasi ya pili inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo ili kuhakikisha inaacha nafasi kubwa ya uwiano wa pointi na kufika 11 ili Yanga itakapocheza michezo yake iliyobakiwa isiwerahisi kuifikia Simba kwa pointi.

Simba leo inwaalika  wajelajela Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam huku ikiwa na kumbukumbu ya kuoata ushindi katika uwanja huo dhidi ya Mbeya City.

Aidha mchezzo huo unaonekana kuwa mgumu kwani Prison imekuwa timu ngumu kufungika hasa katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara na hivyo kuwaoa mashaka wapenzi na mashabiki wa Simba kwa kuhofia kupoteza mchezo huo.

Licha ya kutajwa kuwa ngumu kufungika  nsimu huu prison ina kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa awali uliopiigwa katika uwanja wa Sokonne Mbeya kwa goli 1-0 dhidi ya Simba.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.