Djuma: Wanasimba watafurahi tukiwapa ubingwa
Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Mrundi Masoud Djuma Irambona, amesema ameanza kuunusa ubingwa wa ligi kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Njombe Mji.
Djuma amesema lengo lao la kutwaa ubingwa limeanza kuonekana na wanachohitaji kwa sasa ni kushinda kila mchezo ambao upo mbele yao na ikibidi washinde kwa mabao mengi ili kuzidi kujikita kileleni.
"Tunashukuru Mungu timu inafunga, na tutaendelea kuendelea kushinda kwa nguvu za Mungu na tunaamini tutafaulu, kwa sasa hatuangalii nani yupo nyuma yetu ila ni nani yupo mbele yetu kwa Maana tutacheza na nani," amesema.
Tunakimbizana
"Kwenye Ubingwa tupo tunakimbizana, hatujui mwisho utakuwaje Ila tutakapochukua kombe tutafurahi sana kwani ni miaka mingi timu haipeleki kombe halafu kumezoeleka inawaacha Yanga pointi tisa halafu wao wanakuja kuchukua ubingwa, hivyo itakuwa raha sana kama tukichukua ubingwa," Masoud ameeleza.
Katika mchezo wa uliopigwa katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe April 3, 2018 Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Njombe Mji mabao yote mawili yakifungwa na John Raphael Bocco.
Kwa sasa Simba inaongoza wakiwa na alama 49 alama tatu nyuma ya mahasimu wao wakubwa Dar Young Africans ambao wanaalama 46 katika nafasi ya pili.
Mechi ijayo Simba watakuwa ugenini katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kucheza na wababe wa soka kutoka mji kasoro bahari, Wanatam Tam Mtibwa Sugar.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.