Singida United Yaipiku Yanga Kwa Nyota Huyu, Yatambulisha Wengine Wawili Wa Kimataifa Mmoja Kutoka Brazil.
Winga wa Ndanda FC Tiber John amesajiliwa na klabu ya Singida United, timu hiyo imethibisha leo mbele ya waandishi wa habari.
Yanga ilikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zinamuwania winga huyo kabla ya kuachana nae na kuamua kumrejesha Mrisho Ngassa.
Tiber ni mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji vya hali ya juu.
Mbali na Tiber, Singida United imetambulisha wachezaji wengine wawili iliyowasajili, Felipe Olveira do Santos raia wa Brazil na Amara Diaby, raia wa Ivory Coast.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.