Simba Tayari Wamewasili Kenya

 

Msafara wa wachezaji 18 na viongozi 10 wa kikosi cha Simba umewasili salama jijini Nairobi nchini Kenya tayari kwa michuano ya SportPesa Super Cup.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara watashiriki michuano hiyo inayoanza Jumapili ijayo, Juni 03.

Simba itashuka dimbani Juni 04 kucheza na K. Sharks kwenye dimba la Fraha mchezo ukitarajiwa kuanza saa tisa Alasiri.

Kikosi cha Simba kilichosafiri kuelekea jijini Nairobi, Kenya tayari kwa michuano ya SportaPesa Super Cup
1. Aishi Manula
2. Said Mohamed
3. Ally Salim
4. Ally Shomary
5. Paul Bukaba
6. Erasto Nyoni
7. Yusufu Mlipili
8. Mohamed Hussein
9. Jonas Mkude
10. Shomari Kapombe
11. Mzamiru Yassin
12. Marcel Kaheza
13. Moses Kitandu
14. Rashid Juma
15. Said Hamis Ndemla
16. Haruna Niyonzima
17. Shiza Kichuya
18. Mohamed Ibrahim

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.