NGOMA AFRICA BAND NA CD YAO MPYA AWAMU YA TANO HAPA KAZI
Si wengine ni ile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ,inayoongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras makunja wenye makao yao nchini Ujerumani,bendi hiyo iliyojizolea umarufu kila kona barani ulaya na kufanikiwa kuteka washabiki kwa kutumia muziki wao wa dansi wa bongo.
Ngoma Africa band ukipenda waite FFU ughaibuni au viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" mara hii wamepakua CD yao "Awamu Ya Tano Uwanjani" yenye nyimbo mbili za "Amkeni Kumekucha" na "Awamu ya Tano Sasa Kazi" nyimbo hizo ni utunzi na uimbaji wake Kamanda Ras Makunja akimshirikisha Chris-B Bakotesa ambaye pia ni solo gitaa na kundi zima la FFU wa Ngoma Africa band wakisindikiza kwa mdundo mzima wa Hapa Kazi Kumpigia Saluti na kumuunga mkono Rais Magufuli.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.