TFF INAWABEBA SIMBA


HII NIMEITOA INSTAGRAM KWENYE AKAUNTI YA  (yanga sc group of Supporters)

Nimesikia taarifa ya mchezo wa simba dhidi ya Njombe mji ambao Ulikuwa uchezwe Jumapili tarehe 11/03/2018 umesogezwa mbele. Sababu inayo tolewa ni kuwapa simba muda wa kutosha kufanya Maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho.

Kati hali ya kushangaza kabisa Yanga amecheza leo, Ikumbukwe kuwa Yanga naye anamchezo wa kimataifa dhidi ya Township Rollers Fc tarehe 17/03/2018.


KWANINI TFF INAWABEBA SIMBA ??.
Yanga kabla ya mechi ya kwanza ya Caf Champions League ilicheza siku tatu kuelekea mchezo huo, baada ya mchezo huo tulienda kucheza Songea dhidi ya Maji Maji kombe la FA.


Ratiba ya simba na Yanga .

Tarehe 10/02/2018

Yanga Sc vs St Louis .

Tarehe 11/02/2018

Simba vs Ngendarmerie .

Baada ya siku 3 .

Tarehe 14/2/2018

Yanga Sc vs Maji Maji .

Tarehe 15/02/2018

Simba vs Mwadui Fc .

Tarehe 21/2/2018

St Louis Vs Yanga Sc

Tarehe 20/2/2018

Gendamarie Vs Simba .

Tarehe 25/02/2018

Maji Maji vs Yanga Sc (FA) .

Tarehe 28/02/2018

Ndanda Fc vs Yanga Sc.

Baada ya siku 9 simba anarudi tena uwanjani kucheza dhidi ya Stand United, mechi ilirudishwa nyuma ili simba afanye maandalizi dhidi ya al masry. .

Tarehe 2/03/2018

Simba vs Stand United

Yanga alitakiwa kucheza na Mtibwa Sugar tarehe 1/03/2018. Hiyo ingefanya Yanga acheze mechi 6 ndani ya siku 19, wakati huo Simba akiwa amecheza michezo 4 ndani ya siku 20.

Tarehe 06/3/2018
Yanga Sc vs Township Rollers

Tarehe 07/3/2018

Simba vs Almasry

Tarehe 9/03/2018

Yanga vs Kagera sugar

*Tarehe 11/3/2018*

Ndanda vs Simba.... Mechi imesogezwa mbele kuipa Simba muda wa kufanya Maandalizi.

Kwa hali ilivyo simba inabebwa sana katika ratiba hii ya ligi. Kinacho fanyika ni simba kucheza mechi za Yanga wakati huo huo ikiomba Tff isogeze mbele ratiba ya ligi kuu. Mchezo unao fuata wa simba ni tarehe 17/03/2018 siku nane kutoka leo. Hivi kuna haja gani ya kupoteza siku hizi 8 bila simba kucheza kwa kisingizio cha maandalizi????? Simba wanaogopa kucheza mechi ya ligi kwa kuwa Yanga inawapumulia kwenye usukani. Huu ndio upangaji wa matokeo kwa njia ya kisasa kabisa. Tabia hii inaanza ili kuwapa simba ubingwa wa ligi.

Tff acheni kuwabeba simba, ratiba ya ligi haiwezi.....

Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.