Kwa Wale Mnaobet, Timu Pekee Unayoweza Kubet Na Isikuchanie Mkeka Ni Lipuli Pekee.
"Kwa Wale Mnaobet, Timu Pekee Unayoweza Kubet Na Iskuchanie Mkeka Ni Lipuli Pekee." Hii ni kauli ya msemaji wa klabu ya Lipuli FC, Cement Sanga aliyoitoa kabla ya klabu yake kuianza safari kuelekea Songea kuwakabili Majimaji FC.
Kauli imetolewa mara baada ya matokeo ambayo klabu hiyo imekuwa ikiyapata kwa siku za hivi karibuni hususani katika michezo mitatu ya mwisho ya ligi kuu Tanzania bara ambayo klabu hiyo imefanikiwa kuchukua pointi 7 katika michezo hiyo.
Mara baada ya timu hiyo kuianza safari yake kuelekea Mkoani Ruvuma msemaji huyo ameingeza kwa kusema kuwa wamekwenda Ruvuma kuhakikisha wanaihakikishia Majimaji tiketi ya kuirejesha kunako ligi daraja la kwanza na kuahidi kuinyuka na kuondoka na pointi tatu Ugenini.
TIMU YETU LEO IMEANZA SAFARI KUELEKEA MKOANI RUVUMA KUCHEZA MCHEZO MWINGINE MUHIMU WA LIGI KUU DHIDI YA MAJIMAJI YA SONGEA SIKU YA JUMAPILI.KIKOSI KILICHOONDOKA NDICHO KILICHOPANDA MBEGU YA FURAHA NA MATUMAINI KTK MIOYO YETU KTK MICHEZO MITATU ILIYOPITA HAPO NYUMBANI.KIKOSI KIMEKAMILIKA NA KINA MATUMAINI MAKUBWA YA KUIPOKA MAJIMAJI ALAMA 3...
Aidha Sanga ameendelea kuwasisitiza wakazi, wapenzi, mashabiki na Wanachama wa Lipuli na waoenzi wa soka wa Nyanda Za Juu Kusini kubet kwa Lipuli kwani Ndio Timu pekee isiyoweza kuchana Mkeka Wao.
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.