Mbwana Samatta apiga hattrick yake ya kwanza Ulaya


sokakiganjani
Historia imeandikwa siku ya leo baada ya mshambuliaji kutoka nchini Tanzania Mbwana Ally Samatta kufunga hattrick yake ya kwanza katika michuano ya soka barani Ulaya Europa.



Samatta alikuwepo uwanjani wakati chama lake la Genk likiwakaribisba Brondby katika mfululizo unaondelea wa mechi za kufudhu kwa hatua ya mechi za Europa League.
Dakika ya 37 Samatta aliiandikia Genk bao la kuongoza kabla ya Brondby kusawazisha kupitia kwa Hermannsson, dakika ya 45+1 Genk walifunga bao la pili kupitia Trossard kwa mkwaju wa penati.

Kipindi cha pili Wilszek aliufanya mchezo kuwa 2-2 baada ya kuisawazishia Brondby lakini Samatta tena akafunga dakika ya 55 na 70 kisha Trossard tena na mchezo kuisha 5-2.
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizi mbili unatarajiwa kupigwa Agost 30 ili kumpata anayekwenda Europa

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.