Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 24.08.2018 Mbappe, Rodrigo, Mourinho, Lookman, Rakitic,
Jose Mourinho
amewaambia rafiki zake kwamba angeweza kujiuzulu kutoka klabu nyingine
yoyote kufikia sasa ila Manchester United. Kocha huyo mwenye umri wa
miaka 55 anaarifiwa kutafshika kwa anachokiona kuwa ni ukosefu wa
kuungwa mkono na kaimu mwenyekiti Ed Woodward. (Mirror)
Licha ya kutafshika, Mourinho anasalia kuwa na uwajibikaji mkubwa katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Manchester Evening News)Aliyekuwa mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ana hamu kuipata nafasi kuiongoza Manchester United iwapo tu Mourinho ataondoka. (Mail)
Bin amu wa mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour ameshindwa kuinunua Liverpool kwa thamani ya £ bilioni 2b. (Mail)
Danny Rose wa Tottenham analengwa na Paris St-Germain wanaotaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Mirror)
Real Madrid bado inashughulika kumsajili mchezaji atakayeichukua nafasi ya Cristiano Ronaldo na inaamini ina nafasi ya kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, aliye na miaka 19. (Marca - kupitia Metro)
Klabu hiyo ya Uhispania sasa inahisi 'huenda haitowezekana' kumsajili mojawapo ya washambuliaji wakuu katika ligi ya England katika dirisha hili la uhamisho na sasa wanaelekeza azma yao kwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Valencia Rodrigo, kando na Mbappe. (Independent)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool Iago Aspas, 31, anahitajika na Real Madrid na huenda akaondoka Celta Vigo kwa mkataba wa thamani ya £ milioni 35. (Super Deporte - kupitia HITC)
Real Betis wamewasilisha rasmi ombi la kumsajili mchezaji chipukizi wa Manchester City mwenye umri wa miaka 21 Oleksandr Zinchenko kwam kataba wa mkopo kwa msimu mzima, kwa mtazamo wa kumpa mkataba wa kudumu. (Mundo Deportivo - kupitia Manchester Evening News)
Barcelona inajitayarisha kupokea ombi la thamani ya £81m kutoka Paris St-Germain kwa mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Croatia Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 30. (Sport - kupitia Daily Express)
Meneja Marco Silva anasema winga wa Everton Ademola Lookman ndio 'mustakabali wa wa klabu hiyo' katika jitihada za kuishawishi RB Leipzig kuacha kumfukuzia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Independent)
Kocha mkuu wa Lyon Bruno Genesio anasema mchezaji wa kiungo cha kati anayeshambulia Nabil Fekir, 25, ameona vigumu kukubali kuwa uhamisho wake msimu huu wa joto kwenda Liverpool hakufanikiwa. (Liverpool Echo)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Harrison Reed anaonekana kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo huku Blackburn ikionyesha hamu ya kumchukua mchezaji huyo wa miaka 23 raia wa England. (Daily Echo)
Manchester United haina wachezaji wowote wanaoweza kuingia katika timu ya Jurgen Klopp Liverpool anasema aliyekuwa mshambuliaji wa Reds Dean Saunders. (Talksport)
United inaonekana kuwa tayari kuwapiku wapinzani Manchester City katika kumsajili Lukasz Bejger, mwenye umri wa miaka 16, kutoka Lech Poznan. (Manchester Evening News)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum amefichua namna meneja Jurgen Klopp alivyomtaka kujiimarisha kwa 'kujihusisha zaidi' na kuonyesha ukakamavu msimu huu. (Liverpool FC)
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.