Waamuzi kutoka Afrika watakaochezesha kombe la dunia


Waamuzi sita kutoka barani Afrika, ni miongoni mwa Waamuzi 36 wa Kati, watakaochezesha miaka ya kombe la dunia nchini Urusi kuanzia wiki hii.
Miongoni mwa Waamuzi hao ni pamoja na Abid Charef Mehdi kutoka Algeria.
Wengine ni pamoja na Diedhiuou Malang kutoka Senegal, Gassama Bakary Papa kutoka Gambia, Grisha Ghead raia wa Misri, Sikazwe Janny wa Zambia na Tessema Weyesa Bamlak raia wa Ethiopia.
Said Belqola raia wa Morocco, alikuwa mwafrika wa kwanza kuchezesha fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 kati ya Brazil na Ufaransa.
Belqola alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 45, baada ya kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu.
Mashindano ya mwaka huu pia yana waamuzi wengine wasaidizi 63 huku bara la Afrika likiwakilishwa na waamuzi tisa.
Waamuzi wasaidizi hao ni pamoja na Achik Redouane (Morocco), Ahmed Waleed (Sudan) Birumushahu Jean Claude (Burundi), Camara Djibril (Senegal), Dos Santos Jerson Emiliano (Angola), Etchiali Abdelhak (Algeria), Hmila Anouar (Tunisia), Samba El Hadji Malick (Senegal) na Siwela Zakhele Thusi (Afrika Kusini).