Jerry Muro Amwaga Kinachoiangamiza Yanga.


Afisa Habari wa zamani katika klabu ya Yanga, Jerry Muro, amefunguka na kueleza kuwa suala la uongozi wa timu hiyo kumuondoa aliyekuwa kocha wake, Mholanzi, Hans van der Plujim kimizengwe ndiyo limeifikisha Yanga hapo ilipo.

Muro ameeleza kuwa dhambi na zinawatafuna viongozi wa Yanga waliopo madarakani hivi sasa akisema ndiyo wamesababisha timu kuyumba.

Mbali na hayo, Muro amesema yupo tayari kuchukiwa na wadau wa Yanga akiona ni vema auseme ukweli kwa kuibua mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakifanyika ndani ya klabu.

Hatu hiyo imekuja kufuatia Yanga kuyumba kiuchumi na baadhi ya wachezaji wakihusishwa kuhama kuelekea mahala pengine kutokana na klabu kukumbukwa na hali ngumu kifedha.

"Ndugu zangu wa Yanga Sc niseme wazi hata kama mtanichukia ni heri nichukiwe Kwa kusema ukweli, kuna mambo mengine yanakwenda kwa laana, Kuna dhambi ambayo inawatafuna na itawatafuna sana hata akisajiliwa Cristiano Ronaldo Bado itawatesa sana"

"Kitendo cha kinyama na kihuni mlichomfanyia Babu Hans head coach wa Yanga Sc Kwa kumuondoa kwa mizengwe nasema wazi hapa hiyo laana itawatesa sana, nasema haya kwa kuwa nilikuwa najua kinachofanywa lakini sikuwa na uwezo wa kuzuia kisitokee ila iko siku nitawataja wote waliohusika na kuivuruga Yanga na kuifanya kufika ilipofika"

"Kuna Laana wanapata viongozi ambao leo wote hawako salama kuanzia mwenyekiti mpaka makamu Mwenyekiti na wengine ni shauri ya chuki, roho mbaya waliyomfanyia Babu Hans, Tazameni maisha yao binafsi kila mmoja anapambana na jambo lake kwa wakati wake iko siku nitasema tena kwa kishindo tu, Hii laana mtajuta wanasababisha mamilioni ya mashabiki wa Yanga wanakosa raha kwa Ushenzi wa wachache."

NASEMA TABUNI TENA TABUNI.

Ameandika Jerry Murro 

Aliyewahi kuwa Afisa habari wa klabu ya Yanga