Zahera aifuta mechi ya Yanga na Singida United.


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amefuta mchezo wa kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Singidi United mchezo ambao uliokuwa ufanyike Jumatano ya September 05 katika dimba la Lake Tanganyika Kigoma.

-Zahera ambaye kwa sasa yupo kwenye majukumu ya Timu ya Taifa ya DRC Congo amedai mchezo huo unaweza kuwachosha wachezaji na sasa ametoa maelekezo kwa wasaidizi wake kuanza programu ya mazoezi ili kuwaweka fiti wachezaji kujiandaa na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara.

-Wakati klabu ya Yanga ikiufuta mchezo huo tayari klabu ya Singida United ilishaanza safari ya kuelekea Kigoma kwa ajili ya mchezo huo Singida ambao ijumaa ya August 31 walicheza mchezo wa ligi  Kuu dhidi ya Mbao kwa sasa wapo Mwanza wakiendelea na safari ya kwenda Kigoma na jana walicheza mchezo wa kirafiki na Sumve Combine.

-Alipoulizwa mratibu wa mchezo huo Mrisho Bukuku ambaye pia ni mjumbe wa kamati tendaji ya TFF kupitia kanda ya mikoa ya Kigoma na Tabora amesema hajui lolote kwa klabu ya Yanga kukataa kwenda kucheza mchezo huo. Bukuku akadai maandalizi ya mchezo huo yalishakamilika na kinachosubiliwa ni kuchezwa mchezo huo tu.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.