CHIRWA AIPIGIA MAGOTI YANGA


Unaweza usiamini lakini ndiyo imetokea. Yule straika hatari aliyekuwa akiichezea Yanga, Obrey Chirwa, ametuma maombi kwa mabosi wa klabu yake ya zamani akiomba arejee.

Imeelzwa Chirwa ametuma ujumbe huo kwa njia ya sauti kupitia mtandao akiuomba uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, umpe nafasi ya kurejea.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Chirwa amesema huko alipo Misri mpaka sasa hajapewa fedha zake za usajili na timu anayoichezea hivyo anaweza akavunja mkataba muda wowote.

Aidha, taarifa imeeleza huko anakochezea ni mbali na kwao Zambia hivyo kama akirejea hatakuwa na ugumu wa kusafiri kuelekea kwao kutokana na umbali kutokuwa mrefu.

Mchezaji huyo aliondoka Yanga na kutimkia Uarabuni baada ya kushindwa kufikiana mwafaka na mabosi wake wa zamani kuongeza mkataba mwingine

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.