Yanga Waiadhibu Stand United, Waikalia Kooni Simba Sc..


Walikuwa ni Yanga waliotangulia kuliona lango la Stand United mnamo dakika ya 6' kwa goli la kujifunga kutokana na mpira uliopigwa uzuri na Yusuf Muhilu na kugongwa na wachezaji wawili wa Stand huku mlinzi Ally Ally akiunganisha mpira huo na kujaa wavuni.

Dakika ya 12 Ibrahim Ajibu anafanya kazi nzuri kwa kumalizia mpira ulipigwa kutoka nje kidogo ya box na kuihakikishia yanga kuwa kifua mvele kwa magoli 2-0 magoli yaliyodumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kashi kashi za hapa na oale huku Stand united wakionekana kuwa bora zaidi ya Yanga na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara  langoni mwa Yanga bila mafanikio.

Mnamo dakika ya 84' Stand wanapata goli la kufutia machozi kupita kwa Vitalis Mayanga aliyeunganisha krosi safi na kumuacha Riatand akiwa hana la kufanya.

Lakini dakika moja baadaye Yanga wanafanya Shambulizi la kushitukiza na Obrey Chirwa anapachika kimiani goli la 3 na la mwisho katika mchezo huo.


Hadi kipenga cha mwamuzi kinapulizwa  Yanga 3-1 Stand United.

Kwa matokeo haya sasa Yanga wanafikisha pointi 46 ambazo ni sawa na zile za vinara wa ligi hiyo Simba sc lakini watashika nafasi ya pili kutokana na uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.


Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.