Viporo Vya Simba Kizungumkuti


Simba itaanza mazoezi yake baada ya kupita siku nne huku ikiwa mpaka sasa haijulikani itacheza na timu gani kutokana na kuwa na mechi viporo.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre kitaanza kujifua Jumamosi kuelekea maandalizi ya mechi zilizopo mbele yake za Ligi Kuu.

Pia Yanga wanatarajiwa kuwa na mchezo war obo fainali ya Kombe la FA ambapo watawafuata Singida United kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

Hata hivyo ratiba kwa mechi za Ligi Kuu na ile ya Kombe la Shirikisho mechi za zitakazopigwa hivi karibuni ni kama zifuatavyo;


Ratiba:
Ligi Kuu Tanzania Bara
Aprili 06, 2018
Mbao FC         v Lipuli (Saa 10:00 jioni)
Singida United v Mtibwa Sugar (Saa 10:00 jioni)

Aprili 08, 2018
Stand United     v Njombe Mji (Saa 10:00 jioni)
Ruvu Shooting v Prisons (Saa 10:00 jioni)
Mbeya City    v Azam (Saa 10:00 jioni)
Ndanda         v Kagera Sugar (Saa 10:00 jioni)
Mwadui         v Majimaji (Saa 10:00 jioni)

Robo Fainali Kombe la FA
Mar 30, 2018
Stand United    v Njombe Mji     (Saa 10:00 jioni)

Machi 31, 2018
Prisons        v JKT Tanzania     (Saa 8:00 mchana)
Azam FC         v Mtibwa Sugar     (Saa 2:00 usiku)

Apr 01, 2018
Singida United    v Yanga         (Saa 10:00 jioni)

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.