Twende Taifa, Twende Taifa ,Kazi Ni Moja..

Image may contain: 1 person, sitting
Huo ni usemi wa wengi kuelekea pambano kati ya Simba na Al-Masry katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa jioni ya leo kunako uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Katika kuelekea mchezo huo makocha wa simba wamewataka mashabiki na wanachama pamoja na wapenzi wa kandanda nchini kujitokeza uwanja wa taifa kuiunga mkono klabu hiyo itakapokuwa ikiipeperusha mbendera ya taifa leo.

Aidha katika kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa klabu hiyo amesema anazifahamu vyema klabu za ukanda huo....

“Nazifahamu vizuri timu kutoka Misri, zinakuwa bora na zinatumia nguvu kubwa hasa zinapokuwa nyumbani lakini Simba nayo ni timu nzuri.

“Al Masry wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi yao kwahiyo sio timu ya kubeza lakini tumejipanga vilivyo kuhakikisha tunawafunga nyumbani,” alisema Lechantre.

Aidha Mshambuliaji wa Simba anayefanya vizuri ndani ya timu hivi sasa, John Bocco, amesema kuwa Simba ina historia nzuri katika soka la kimataifa.

Bocco amesema hayo kutokana na timu hiyo kuwahi kufika katika fainali ya mashindano ya CAF mwaka 1993 iliyopigwa Shamba la Bibi ama Uwanja wa Uhuru dhidi ya Stella Abdijan.


Aidha mshambuliaji huyo amesema hawakufanya vema katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ya Shinyanga, hivyo amesema watatumia makosa ya mechi hiyo leo dhidi ya Al Masry SC.

Bocco ameeleza ni wakati mwafaka wa kufanya vema mechi ya nyumbani ili wakienda ugenini wasije wakapata ugumu wa kusonga mbele.

Vilevile Bocco hakuishia hapo bali amewaomba mashabiki kujitkkeza kwa wingi kesho uwanjani ili waweze kuipa sapoti timu yao.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.