Manara: Yanga walijitakia wenyewe



Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka kuhusu matokeo ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliowakutanisha Yanga dhidi ya Township Rollers ya Bostwana Jumanne ya leo.
Kupitia kipindi cha E Sports kupitia radio EFM ya Dar es Salaam, Manara amesema Yanga wamepoteza kizembe kutokana na kutumia muda mwingi kuongelea mechi ya Simba tofauti na kujadili namna ipi watapambana na Township Rollers.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya Yanga kupoteza mchezo wa leo kwa mabao 2-1 na kujitengenezea mazingira magumu kusonga kwenye mcheo wa marudiano ambapo Yanga italazimika kushinda mabao matatu kwa 0.
Haji Manara ameshauri pindi panatokokea mechi za kimataifa kama hizi, ni vema vilabu vikaungana kuwa taifa moja na kupeana hamasa badala ya kuleta matabaka.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.