Kuelekea Simba dhidi ya Al-Masry hizi hapa rekodi muhimu za kufahamu.


Huku klabu ya kutoka Tanzania, Simba wakijinasibu kua na rekodi nzuri zaidi dhidi ya timu za kutoka Kaskazini mwa Afrika huenda ikawa ni morali ya kuelekea mchezo wa kesho Jumatano katika kombe la Shirikisho barani Afrika ( CAF Confederation Cup) dhidi ya klabu kutoka Misri, Al Masry lakini ni vyema tukapata uchmbuzi wa takwimu hizi kadhaa kutoka kila upande

- Namna gani kila klabu imefika hatua hii

Simba wamefika hatua hii baada ya kuwafunga kwa jumla ya mabao 5-0 klabu ya  Gendarmerie kutoka Djibouti ambapo walishinda kwa 4-0 nyumbani na kushinda tena kwa 1-0 ugenini.

Al Masry wamefanikiwa baada ya ushindi wa jumla ya mabao 5-2 dhidi ya klabu ya Green Buffaloes wakishinda kwa 4-0 nyumbani huku wakiambulia kipigo cha 2-1 ugenini.

- 'Perfomance' ya kila klabu msimu uliopita

Hii ni kwa mara kwa Simba kushiriki michuano hii baada ya miaka mitano, mara ya mwisho kwa Wanamsimbazi kushiriki michuano ya CAF ilikua mwaka 2012 katika klabu bingwa ambapo walipata kipigo cha bao 5-0 kutoka kwa Recreativo Desportivo Do Libolo ya nchini Angola.

Al Masry wao mara ya mwisho msimu uliopita waliondoshwa na klabu ya KCCA ya nchini Uganda.

- Rekodi za nyumbani na ugenini

Inaonekana Al Masry wanakuwa hatari zaidi wanapokuwa nyumbani, kwa kuanzia msimu uliopita walishinda mechi zao zote tatu katika michuano hii bila kuruhusu bao lolote, hata hivyo hawana rekodi nzuri wanapokuwa ugenini  kwani walifungwa mechi zote bila kuambulia angalau sare.

Simba walifungwa nyumbani na  Libolo mwaka 2012 kwa mabao 4-0, lakini hata hivyo kwa mechi za hivi karibuni wameonekana kua vizuri ambapo mchezo wa kwanza dhidi ya Gendarmerie wakishinda 4-0 huku mchezo wao na Al Masry utakua ni wa tatu wakiwa nyumbani.

- Wachezaji wa kutizamiwa kila upande

Simba walikuwa na msimu mzuri wa usajili kwa kusajili wachezaji kadhaa wazuri kwani kwa sasa wana wachezaji wengi wenye kuweza kubadilisha matokeo mfano kinara wa mabao VPL, Emmanuel Okwi na mshabuliaji 'pacha' mwenzake, John Bocco bila kumsahau Shiza Kichuya ambaye naye sio wa kumchukulia poa.

Ahmed Gomaa na Ahmed Shoukry ni wachezaji wa kuangalia zaidi kwa upande wa Waarabua hao wa Misri kwani wanaonekana kua na 'kombinesheni' nzuri zaidi ambapo wanaweza kuwa hatari zaidi langoni mwa Simba.

KILA LA KHERI WANAMSIMBAZI!!

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.