Taarifa Mpya Kutoka Simba Asubuhi Ya Leo Machi 6.2018
-Kikosi cha Simba sc jana kimefanya mazoezi hadi usiku kuhakikisha kinakuwa imara kuelekea mtanange wa kimataifa dhidi ya Al-Masry utakaopigwa kesho katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam.
-Ikumbukwe kuwa Makocha Hossam Hassan wa Timu ya Al-Masry na Pierre Lechantre wa Simba leo majira ya saa tano asubuhi watazungumza na Wanahabari Kuelekea mchezo wao wa kombe la Shirikisho utakaopigwa siku ya kesho.
Mkutano huo muhimu utafanyika kwenye ukumbi wa Kivukoni four uliopo ktk Hoteli ya Nyota tano ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es Salaam.
-Wakati huo huo Waziri wa kilimo wa Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Charles Tizeba anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanasimba na watanzania kuishangilia Simba kwenye mchezo huo utakaoanza saa kumi na mbili jioni.
Mh Tizeba ndio mgeni rasmi katika mchezo huo ambao utachezeshwa na Waamuzi toka nchini Afrika kusini.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.