Taarifa Mpya 3 Kutoka Yanga Asubuhi Hii.



-Leo ndio leo ile droo iliyokuwa ikingojewa ya upangaji wa timu zitakazokutana kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, inataraji kufanyika leo mjini Cairo, Misri.
Droo hiyo itahusisha timu zilizoanguka kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na timu ambazo bado zipo Kombe la Shirikisho.


Miongoni mwa timu hizo ni pamoja na waliokuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa, Yanga sc leo ndio siku ambayo itaamuliwa kuwa watanzania hao watakutana na Waarabu Al-masry, Raja Cassablanca, Enyimba au SuperSpot United ya Afrika Kusini.

-Taarifa nyingine asubuhi hii ni kuhusu kurejea kwa nyota wa klabu ya Yanga ambao walikuwa na majeruhi wa muda mrefu huku ikielezwa kuwa wako vizuri. Wachezaji hao ni Amis Tambwe na Donald Ngoma.

Hayo yaemwekwa bayana na mkuu wa kitengo cha habari wa klabu hiyo, Dismas Ten .


"Kwa sasa hatuna wachezaji majeruhi. Amissi Tambwe na Donald Ngoma wamekuwa wakifanya mazoezi peke yao, Alhamisi watajiunga na wenzao"



- Ya mwisho asubuhi hii ni ile ya uzinduzi wa huduma za kidigitali.


Yanga imezindua huduma ya kupata habari mbalimbali za Yanga kupitia ujumbe mfupi kwenye simu za mkononi.

Huduma hiyo kwa sasa inapatikana kwenye mtandao wa Tigo ambapo ili uweze kujiunga unatuma neno YANGA kwenda 15501.

Gharama ya ujumbe mfupi ni Tsh 100 tu. 


Aidha imeelezwa kuwa ifikapo Aprili mosi (01.04.208) Yanga itaanza kurusha kipindi maalumu cha Yanga TV Show.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.