Yondani, Tshishimbi Kuongoza Kikosi Cha Wachezaji 20 Yanga Kwenda Kenya.


Kikosi cha wachezaji 20 wa Yanga, wakiwemo Nahodha Kevin Yondan, kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kinaondoka kesho kwenda Kenya kwa ajili ya michuano ya pili ya SportPesa Super Cup.

Katika michuano hiyo inayoanzia hatua ya Robo Fainali, Yanga wataanza na Kakamega Homeboys Juni 4, siku moja baada ya majasimu wao, Simba SC kumenyana na dimba na Kariobangi Sharks Juni 3 na, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Afraha, Nakuru.


Mechi nyingine ni kati ya mabingwa watetezi, Gor Mahia na JKU ya Zanzibar Juni 3 pia na Singida United ya Singida dhidi ya wenyeji wengine, AFC Leopards Juni 5.Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo ataondoka kitita cha dola za Kimarekani, 30,000, mshindi wa pili dola 10,000, wa tatu dola 7,500 zitakazoishia Nusu Fainali dola 5,000 na za Robo Fainali dola 2,500.

Pamoja na dola 30,000, bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu atapata fursa ya kwenda kumenyana na klabu ya Everton nchini England.

Mwaka jana Gor Mahia ilikuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo baada ya kuwafunga mahasimu wao, AFC Leopard 2-1 katika fainali kwenye michuano iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.