Southampton Yamfuta Kibarua Kocha Wake Mkuu "Mauricio"


Klabu ya Soka ya Southampton imethibitisha kuachana na  Meneja wa Timu ya Kwanza Mauricio Pellegrino na hii ni kutokana na matokeo mabovu ambayo imekuwa ikiyapata siku za hivi karibuni.

Aidha klabu hiyo pia imuwaacha Meneja Msaidizi Carlos Compagnucci na Msaidizi wa Timu ya Kwanza Xavier Tamarit.

"Tunapenda kutoa shukrani  kwa Mauricio, Carlos na Xavier kwa juhudi zao wakati walipokuwa Southampton, na tunanawatakia mafanikio mazuri kwa siku zijazo."
 

Klabu itaangalia na kuteua mtu wa  kusimamia haraka iwezekanavyo, huku ikiendelea na kutafuta mrithi wa Mauricio.

Southampton mpaka sasa imecheza mechi 30 na inashikilia nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi kuu England.

Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.