Simba Anakwenda Kubebeshwa 10 Misiri: Kifaru.
Afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amefunguka ya moyoni kuhusiana na vilabu vya Tanzania vinavyoiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.(CAF Champions League na CAF Confederation Cup).
Kwa mujibu wa Kifaru ameiomba serikali kuingiza mkono katika kutoa Support kwa vilabu hivyo ili kuhakikisha uendeshaji katika safari na maandalizi ya kuelekea michezo hiyo. Akizungumza na kituo cha Redio cha Kasibante FM amesema kuwa kutokana na hilo basi wamekosea kwani hatutofanikiwa wala kufika popote.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa timu zetu zinastahili kuwa na maandalizi ya kutosha huku zikiwa na nafasi kubwa ya kufanya ziara katika nchi mbalimbali kwa kucheza michezo ya kujipima uwezo na timu mbalimbali.
"Mimi nashauri kuwa vilabu vyetu vinavyoshiriki michuano ya kimataifa vinakosea huwezi kusema kuifunga Ruvu shooting goli 7 utaenda kimataifa na ukafanya vizuri unajidanganya wala huwezi kusema kuifunga Majimaji goli 4 utaenda kufanya vizuri kimataifa"
"Yanga tayari wameshatolewa huko wanakoenda wanakwenda kutalii tu maana wamepoteza nyumbani huko wanakoenda watapigwa, Simba nao sioni nafasi kama wametoa sare nyumbani wakoenda huko anabeba 10"..
Ikumbukwe kuwa vilabu vya Simba na Yanga zinazowakilisha nchi kimataifa zitashuka dimbani wikendi hii katika miche yao ya marudiano.
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.