Hawa Ndio Wacheza Wa Simba Watakaoondoka Nchini Kwenda Misiri Kuwavaa Al-masry.


-Timu ya Simba Sc itakwea pipa siku ya Jumatano kuwafuata Al Masry ya Misri kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup) na nyota 21 mchezo utaochezwa Jumamosi ya march 17 saa 2:30 usiku.

-Simba wanaenda Misri kutafuta ushindi wa aina yoyote au kutoa sare ya magoli 3+ ili kufuzu hatua inayofuata kwani katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika jijini Dar Simba walilazimishwa sare ya magoli mawili kwa mawili (2-2)

-Habari za kuaminika kutoa Simba zinadai Simba waataondoka na kikosi cha wachezaji 21 kwenda kuwakabili Al Masry ambao ni magolikipa Aishi Manula, Said Mohamed Ndunda, Mabeki ni Shomary Kapombe, Ally Shomary,  Hussein Mohamed, Asante Kwasi, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Juuko Murshid, na Paul Bukaba

-Wachezaji wengini ni viungo, Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto, na Shiza Kichuya huku washambualiaji ni John Bocco, Emmanuel Okwi, Nicholas Gyan, Moses Kitandu na Laudit Mavugo.

Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.