Matokeo Ya Ligi Kuu Ya Tanzania .
Ligi kuu soka Tanzania Bara raundi ya 21 mzunguko wa pili imeendelea tena Alhamis ya Machi 8, 2018 kwa michezo minne iliyopigwa katika viwanja vya miji ya Shinyanga, Songea, Iringa na Dar es Salaam.
Katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, wapiga debe wa Stand United wamefanikiwa kuwalazimisha suluhu ya 0-0 timu ngumu ya Tanzania Prisons ‘wajelajela’.
Matokeo hayo yanawafanya Stand United kufikisha alama 22 na kujivuta hadi katika nafasi ya 11 wakati Tanzania Prisons wao wameendelea kung’ang’ania nafasi ya tano wakiwa na alama 33.
Lipuli 2-1 Njombe
Matokeo mengine Lipuli wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Njombe Mji mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mabao ya Lipuli yamefungwa na Jerome Lambele na Adam Salamba huku lile la kufutia machozi la Njombe Mji likifungwa na David Obash katika dakika ya 33.
Kwa matokeo hayo, Lipuli wanapanda hadi nafasi ya 7 wakiwa na alama 26 kibindoni huku Njombe Mji wakiwa bado wapo katika nafasi mbaya ya 15 na alama zao 18 katika msimamo wa ligi.
Majimaji 0-1 Ndanda
Mkoani Ruvuma, timu ya Majimaji wamefungwa nyumbani na Wanakuchele Ndanda FC kwa bao 1-0 lililofungwa na Tibar John, matokeo ambayo yanazidi kuwaweka pabaya timu hiyo ambayo bado inashika mkia ikiwa na alama 15.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.