Simba Queens Yafumuliwa Tena, Kamata Matokeo Ya Ligi Kuu Ya Wanawake Tanzania..
WPL Super 8
Hatua ya nane bora ya ligi kuu ya wanawake Tanzania Bara imeendelea leo kwa michezo miwili ambapo katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, timu ya soka ya Alliance Queens imefanikiwa kuwaduwaza Simba Queens kwa bao 1-0.
Bao la Alliance Queens limefungwa na Aisha Juma katika dakika ya 18 ya mchezo huo na kuwafanya kufikisha alama 7 katika ligi hiyo inayohusisha mechi za nyumbani na ugenini.
Mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri, Wababe wa ligi hiyo JKT Queens wameishindilia bila ya huruma timu ya soka ya Baobaob Queens kwa mabao 6-0 na kuendelea kujiimarisha kileleni wakiwa na alama 12.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.