Baada Ya Matibabu India Sasa Kurejea Uwanjani Rasmi(Niyonzima)
DAKTARI wa Simba, Yassin Gembe amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba wasiwe na wasiwasi, Haruna Niyonzima atarejea uwanjani baada ya mechi ya Al Masry.
Niyonzima alikuwa India hivi karibuni ambako alitarajia kuwa angefanyiwa upasuaji lakini haikuwa hivyo badala yake alipewa matibabu maalum ya kumrejesha katika hali yake ya kawaida.
Akizungumza na Spoti Xtra, Gembe alisema; “Niyonzima anaendelea vizuri tunashukuru hilo lakini suala la yeye kuanza mazoezi rasmi na kikosi hii itakuwa ni baada ya siku zijazo.”
“Hivyo kuungana na timu itakuwa ni baada ya mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry ambayo itachezwa huko Misri wakati timu itakaporejea ndiyo atakuwa na uwezo wa kuanza mazoezi na wenzake tofauti na hapo wachezaji wengine wanaendelea vyema,” alisema Gembe.
Hiyo inamaanisha kwamba mpaka kuja kufikia mechi ya watani wa jadi mchezaji huyo atakuwa amesharejea uwanjani.
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.