Achana Na PCM, KIBO Wanatisha.


Safu ya ushambuliaji ya klabu ya Simba imekuwa ndio safu bora katika upachikaji wa magoli katika michuano mbalimbali msimu huu huku ikicheza michezo michache zaidi.

Kwa mujibu wa takwimu safu ya Ushambuliaji ya Yanga (PCM) Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa na Emmanuel Martine imecheza michezo 26 na kufanikiwa kupachika magoli 21 pekee ilihali wapinzani wa Simba (KIBO) Kichuya,Bocco na Okwi wao wameshuka dimbani katika michezo 24 na kupachika Kambani magoli 40.

Kwa idadi hiyo ya magoli ya safu hiyo ya ushambuliaji ya Simba yanakuwa ni magoli mengi zaidi ya yake yaliyofungwa na wachezaji wote wa klabu ya Yanga.


Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.