Yanga Kuwafuata Majimaji Kesho Kwa Pipa...


Baada ya kurejea nchini Yanga leo watafanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, kilichopo Kurasini mjini Dar es Salaam kabla ya mapema kesho kusafiri kwa ndege kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Jumapili.

Hatua ya 16 Bora ya ASFC itaendelea leo kwa Singida United kuwakaribisha Polisi Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida na KMC kumenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mbali na Maji Maji na Yanga, mechi nyingine za Jumapili ni Buseresere FC watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na JKT Tanzania watakaomenyana na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi za 16 Bora ya ASFC zitakamilishwa Jumatatu ya Februari 26, Kiluvya United wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Stand United watakuwa wenyeji wa Dodoma FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.