Mpya Kutoka Simba Sc Leo Ijumaa .


Kikosi cha Simba leo jioni kinatarajiwa kuaanza tena mazoezi tayari kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Mbao FC. 

Kikosi cha Simba kilipewa mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Djibout katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gendarmerie ambapo kikosi cha Simba kilishinda kwa goli 1-0 na hivyo kujiandikishia tiketi ya kwenda hatua ya mbele zaidi. 

Mazoezi leo jioni yataanza saa 10:00 katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.